2022/12/12 by Ba, Mame-Penda, Cury, Philippe
paper · doi:10.57832/e887-0597
Changamoto zinazoikumba sayari yetu, mabadiliko ya tabianchi, kupotea kwa uwingi wa viumbe na mimea, kuzuka kwa magonjwa mapya, hayo yote yanahitaji mbinu zinazoundwa na watu husika katika maeneo husika, katika muktadha wa utandawazi. Matatizo na vizuizi hivyo vinatupa nafasi ya kufikiri upya mageuzi ya kiuchumi, kimazingira, na kijamii yanayotakikana ili kufanikisha maendeleo endelevu, kulingana na Ajenda ya 2030. Leo, tunahitaji sayansi za maarifa na sayansi za uvumbuzi ili tuweze kutathmini vizuri iwezekanavyo nyuso za nyakati zijazo, vizuizi vya kisayari ambavyo tutalazimika kuishi navyo, na pia kuunda mbinu mpya zitakazoweza kutumika katika maeneo mbalimbali, yakiwa ya ndani au ya kikanda kwa jumla. Ni lazima tafiti za kiafrika za sayansi zitumie nguvu takiwa ili kukabiliana ipasavyo na changamoto hizi. Changamoto hizi zinatuhimiza kubuni upya namna utafiti unaweza – na unapaswa – kuchangia, kwa kujikita kwenye malengo hayo, kwa kuipa kipaumbele sayansi endelevu itakayowezesha fani mbalimbali kutumia maarifa zote zilizonazo kutimiza lengo la maendeleo. Kutekeleza mageuzi yake yenyewe kwa sera zake, utafiti wake, malengo yake ya muda mfupi na ya kati, kunahitaji utafiti unaoweka mbele dhana ya bara la Afrika linalong’aa kwenye uwanja wa kimataifa, utafiti utakaoyafanyia kazi malengo ya kiafrika katika kuhakikisha maendeleo endelevu.